Mkuu wa Idara ya mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dkt. Amani Sanga amesema zoezi la upigaji chapa mifugo (Ng'ombe) kwa Halmashauri hiyo linaendelea ambapo mpaka sasa jumla ya Ng'ombe elfu 8,652 wamepigwa chapa ya moto na kuvalishwa Hereni kwenye Vijiji vya Majengo Kati, Kaloleni, Ambureni, Moivaro, Sura ,Kimundo,Sing'isi,Poli,Maji ya chai,Ngyani,Nkure Sangananu na Olkung'wado, aidha ameeleza zoezi hili la upigaji chapa ni utekelezaji wa agizo la Serikali la kuhakikisha Mifugo yote inaingizwa kwenye mfumo wa utambuzi na ufuatiliaji wa mifugo Tanzania (TANLISTS) ifikapo tarehe 31 Januari 2018.
Dkt.Sanga amesema zoezi hilo litawezesha udhibiti wa wizi wa mifugo,kuthibiti uhamishaji wa mifugo pia litazuia kusambaa kwa magonjwa ,kudhibiti ubora wa mifugo na mazao yake pamoja na kusaidia upatikanaji wa masoko ya mifugo na mazao yake.
Mwananchi aliye jitambulisha kwa jina moja Danieli ambaye ni mfugaji mkazi wa Kijiji cha Olkung'wado Kata ya Ngarenanyuki ambapo zoezi la upigaji chapa limefanyika amesema "zoezi hili la uwekaji alama mifugo yetu ni zuri na litatusaidia kudhibiti uwizi wa mifugo ,nawashauri Watanzania wote kushiriki zoezi hilo kwani kutofanya hivyo ni kukaidi agizo la Serikali hivyo watapewa adhabu"
Asanterabi Urasa ambaye ni Afisa Mifugo amesema zoezi hilo la usajili,utambuzi na ufuatiliaji wa Mifugo(Ng'ombe) unatofautiani kati ya Ng'ombe wa Maziwa na Ng'ombe wasio wa maziwa kwa kufafanua kuwa Ng'ombe wasio wa maziwa wanapigwa chapa ya maandishi (moto) tofauti na Ng'ombe wa Maziwa kupitia mradi wa kuboresha koo za Ngombe wa Maziwa(ADGG) husajiliwa kwa kuvishwa Hereni ,ameongeza kua Wafugaji wa Ngombe wa maziwa ambao waliosajiliwa watakua wakitembelewa na wataalamu wa mifugo watakaochukua taarifa mbalimbali za ufugaji aidha taarifa hizo zitachakatwa na mfugaji aatapewa mrejesho kupitia simu yake ya Mkononi lengo likiwa ni kuelimisha ufugaji wa Ng'ombe wa Maziwa kwa tija. .
Afisa Mifugo wa kata ya Ngarenanyuki Jasper Soi amewasihi Wafugaji wa Kata hiyo kuhakikisha Mifugo yao inapigwa chapa kabla ya tarehe 01 Februari 2017 kwa kuzingatia ratiba iliyotelewa kwa kila kijiji.
Ikumbukwe kua sheria na 26 ya mwaka 2010 ,sheria ya utambuzi,usajili na ufuatiliaji wa mifugo inatumika kutoa adhabu ya kulipa faini ya kiasi cha Milioni 2,kifungo cha Mwaka Mmoja au vyote kwa pamoja kwa mtu yoyote asiye piga chapa mifugo au atakayekwamisha kwa njia yoyote zoezi la upigaji chapa .
PICHA ZA ZOEZI HILO
Mifugo ya Wanakijiji wa Kijiji cha Olkugw'ado Kata ya Ngarenanyuki wakiwa kwenye maandalizi kwaajili ya kupigwa chapa
Maafisa Mifugo wa Halmashauri ya Meru ,Joe Hiza (kulia) na Jasper Soi kushoto wakipasha moto vyuma vyenye alama ya utambuzi ya Kijiji cha Olkug'wado kwaajili ya Kuwapigia chapa mifugo ya kijiji hicho.
Afisa Mifugo wa Kata ya Ngarenanyuki Jasper Soi akimpiga chapa Ng'ombe wa Mfugaji katika kijiji cha Olkung'wado
Danieli ambaye ni mfugaji amkazi wa Kijiji cha Olkung'wado Kata ya Ngarenanyuki ambapo zoezi la upigaji chapa limefanyika .
Afisa mifugo Mwagilo Mbelwa akiwa amejiandaa kupiga chapa Ng'ombe wa wafugaji wa Kijiji cha Olkungwado.
Afisa mifugo Mwagilo Mbelwa akiwa amejiandaa kupiga chapa Ng'ombe wa wafugaji wa Kijiji cha Olkungwado.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa