Halmashauri ya Meru ina eneo la ukubwa wa mita za mraba 8,443 lililopo mbele ya Ofisi za Makao Makuu ya Halmashauri ambalo linafaa kwa ajili kuanzisha Bustani ya kupumzikia ya wananchi.
Bustani hii inaweza kufanyiwa Landscaping kwa mbele karibu ya barabara ya Lami kuonyesha taswira ya Mlima Meru kama ilivyo kwa eneo la Makao Makuu ya EPZ, Mabibo Jijini Dar Es Salaam.
Nyuma ya mlima huo kunaweza kujengwa chumba cha kuonyesha bidhaa za utamaduni wa Wameru na pia kukawa na Mgahawa kwa ajili ya kuhudumia watu watakaotembelea eneo hilo. Eneo lingine linalobaki linakuwa na viti vya kupumzikia chini ya miti ya asili iliyopo.
Miundombinu ya maji, umeme iko jirani lakini pia eneo hili liko pembeni ya barabara ya lami (Arusha-Moshi).
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa