Sekta ya Elimu Sekondari
Halmashauri ya Wilaya ya Meru ina jumla ya shule 57 za Sekondari, kati ya hizo Shule 29 zinamilikiwa na Serikali na Shule 28 zinamilikiwa na taasisi zisizo za Serikali. Katika shule 29 za serikali, shule tatu (3) zina kidato cha Tano na Sita ambazo ni Maji ya Chai, Kisimiri na Makiba.
Aidha shule zisizokuwa za serikali zenye kidato cha Tano na Sita ni pamoja na St.Mary’s Duluti, Makumira, Mariado, Usa River Seminary, Ailanga, Star High school, Ngarenanyuki, Tanzania Adventist, Hebron na Jude Moshono.
1.1 Idadi ya Walimu
Halmashauri ya Wilaya ya Meru ina jumla ya walimu 1,318 katika shule za Sekondari za serikali kwa takwimu za Mei, 2017 kwa mchanganuo ufuatao:-
Jedwali Na. 1: Mahitaji ya walimu kwa masomo
MASOMO
|
MAHITAJI
|
WALIOPO
|
UPUNGUFU
|
ZIADA
|
Sayansi na Hisabati
|
204
|
139
|
65
|
0
|
Biashara
|
24
|
12
|
12
|
0
|
Sayansi ya Jamii
|
705
|
1155
|
00
|
450
|
Jumla
|
910
|
1,318
|
77
|
450
|
Aidha mwezi APRIL 2017 Serikali iliajiri walimu wapya wa Sayansi na Hisabati ambapo Halmashauri ilipangiwa walimu 11 kati ya hao walimu 10 wameripoti vituoni na tayari wameanza kazi.
1.2 Uandikishaji Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza 2017
Jumla ya wanafunzi 4,352 (wavulana 1964, wasichana 2,388) wamechaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwaka 2017. Hadi tarehe 17 Mei, 2017 wanafunzi ambao wamekwisha kuripoti shuleni ni wanafunzi 3,551 (Wavulana 1572 na wasichana 1979) ambao ni sawa na 84% ya wanafunzi wote waliochaguliwa.
Aidha kulikuwa na changamoto katika kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza, ikiwemo upungufu wa madarasa, viti na meza. Hatua zilizochukuliwa katika kukabiliana na changamoto tajwa ni pamoja na kutumia Tsh.62,492,300 za mapato ya ndani kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 15 kwenye shule zenye upungufu. Pia kiasi cha Tsh.19,684,384 kutoka mapato ya ndani kimetumika kwa ajili ya kununua meza/viti 328 kwa ajili ya wanafunzi.
1.3 Mahitaji ya Miundo Mbinu
Mahitaji ya Miundombinu ya elimu ambayo ni vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, ofisi, vyoo vya wanafunzi na walimu ni kama yanavyoonekana hapo chini.
Jedwali Na. 2: Miundombinu ya shule za sekondari.
Aina ya Miundo Mbinu
|
Mahitaji
|
Yaliyopo
|
Upungufu
|
Maabara
|
87 |
56 |
31 |
Nyumba za Walimu
|
910 |
96 |
814 |
Jengo la Utawala
|
29 |
19 |
10 |
Vyumba vya Madarasa
|
361 |
319 |
42 |
Matundu ya Vyoo.
|
613 |
392 |
221 |
Maktaba
|
29 |
5 |
24 |
1.4 Meza na Viti vya wanafunzi
Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa sasa ina idadi ya wanafunzi 11,736 hivyo kufanya mahitaji ya meza na viti kuwa11,736. Aidha kuna baadhi ya shule ndani ya Halmashauri zina upungufu wa viti 935 na meza 786 lakini pia kuna baadhi ya shule ndani ya Halmashauri zina ziada ya viti 2,185 na meza 1,892. Shule hizi zipo katika kata tofauti tofauti hivyo ni changamoto kuhamisha viti au meza kutoka shule moja kwenda shule nyingine kwa kuwa samani hizi zilitengenezwa kwa nguvu ya jamii za kata husika. Ili kukabiliana na changamoto hii viti/meza za ziada zimehamishwa kutoka shule zenye utoshelevu kwenda kwenye shule zenye upungufu.
Jedwali Na. 3
Idadi ya Shule
|
29 |
|||||||
Idadi ya Wanafunzi
|
11,736 |
|||||||
Idadi ya Samani
|
MAHITAJI
|
YALIYOPO
|
UPUNGUFU
|
ZIDIA
|
||||
VITI
|
MEZA
|
VITI
|
MEZA
|
VITI
|
MEZA
|
VITI
|
MEZA
|
|
11736
|
11736
|
12986
|
12945
|
935
|
786
|
2185
|
1892
|
1.4 TAARIFA YA KINA KUHUSU MIRADI YA ELIMU SEKONDARI
Jedwali Na.4
S/N |
AINA YA MRADI |
MAHALI ULIPO |
MWAKA ULIPOANZA |
GHARAMA ZA MRADI |
WAHUSIKA WA GHARAMA |
JINA LA MRADI
|
GHARAMA ZA KUKAMILISHA
|
HATUA YA MRADI
|
WANUFAIKA
|
1 |
UJENZI WA MADARASA 2, NYUMBA MOJA YA WALIMU (SIX IN ONE) MATUNDU MAWILI(2 STANCES) NA MATUNDU MANANE YA WANFUNZI ( 8 STANCES) |
MALULA SEKONDARI |
2014/15 |
221,637,000 |
WORLD BANK |
MMES II
|
221,637,000
|
MRADI ULIKAMILIKA
|
WANAFUNZI 80 WALIMU SITA NA WANAFUNZI 331 WA SEKONDARI MALULA
|
2 |
UJENZI WA MADARASA 2, NYUMBA MOJA YA WALIMU (SIX IN ONE) MATUNDU MAWILI(2 STANCES) NA MATUNDU MANANE YA WANAFUNZI ( 8 STANCES |
MOMELA SEKONDARI |
2014/15 |
222,000,000 |
WORLD BANK |
MMES II
|
222,000,000
|
MRADI ULIKAMILIKA
|
WANAFUNZI 80 WALIMU SITA NA WANAFUNZI 387 WA SEKONDARI MOMELA
|
3 |
UJENZI WA MATUNDU 8 YA VYOO VYA WANAFUNZI ( 8 STANCES) NA MATUNDU MAWILI YA WALIMU( 2 STANCES) |
KITEFU |
2014/15 |
20,000,000 |
WORLD BANK |
MMES II
|
20,000,000
|
MRADI ULIKAMILIKA
|
WANAFUNZI 240 NA WALIMU 42 WA SHULE YA SEKONDARI KITEFU
|
4 |
UJENZI WA MADARASA MAWLI ( 2 CLASSROOMS) MATUNDU 8 YA VYOO VYA WANAFUNZI ( 8 STANCES) |
LAKITATU SEKONDARI |
2014/15 |
64,423,500 |
WORLD BANK |
MMES II
|
64,423,500.00
|
MRADI UMEKAMILIKA
|
WANAFUNZI 275 WA SHULE YA SEKONDARI LAKITATU.
|
5 |
UJENZI WA MATUNDU MAWILI YA VYOO VYA WALIMU |
POLI SEKNDARI |
2016/17 |
4,907,654.47
|
WORLD BANK |
P4R
|
4,907,654.47
|
MRADI UKO KATIKA HATUA YA UKAMILISHAJI
|
WALIMU 45 WA SHULE YA SEKONDARI
|
6 |
KUKAMILISHA MIUNDO MBINU YA MAABARA MOJA |
SAKILA SEKONDARI |
2016/17 |
6,756,379.60 |
WORLD BANK |
P4R
|
6,756,379.60
|
MRADIUMEKAMILIKA
|
WALIMU 45 WA SHULE YA SEKONDARI
|
7 |
KUKAMILISHA MIUNDO MBINU YA MAABARA MOJA |
LAKI TATU SEKONDARI |
2016/2017 |
6,500,000.00 |
WORLD BANK
|
P4R
|
6,500,000.00
|
MRADI UKO KATIKA HATUA YA UKAMILISHAJI
|
WANAFUNZI 241 PAMOJA NA WALIMU 38
|
8 |
KUKAMILISHA VYUMBA VIWILI VYA MADARASA |
NKOANEKOLI SEKONDARI |
2016/2017 |
11,000,000.00 |
WORLD BANK |
P4R
|
11,000,000.00
|
MRADI UKO KATIKA HATUA YA UKAMILISHAJI
|
WANAFUNZI 178 WA SHULE YA SEKONDARI MIRIRINI
|
9 |
UJENZI WA MATUNDU 8 VYOO VYA WANAFUNZI |
MIRIRINI SEKONDARI |
2015/2016 |
22,284,600 |
WORLD BANK |
P4R
|
22,284,600.00
|
MRADI UMEKAMILIKA
|
WANAFUNZI 106 WA SHULE YA SEKONDARI NKOANEKOLI
|
10 |
UJENZI WA MABWENI 2,VYUMBA VYA MADARASA 8 NA MATUNDU 20 YA VYOO VYA WANAFUNZI. |
KISIMIRI SEKONDARI |
2016/17 |
480,000,000.00 |
WORLD BANK |
P4R
|
480,000,000.00
|
MRADI UMEKAMILIKA.
|
|
1.6 Taaluma na Ufaulu
Kulingana na takwimu za Baraza la mitihani Tanzania (NECTA), ufaulu wa kidato cha nne (CSEE) kwa miaka mitatu iliyopita ni kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini.
Jedwali Na. 6: Ufaulu wa Kidato cha nne kuanzia mwaka 2013 hadi 2016
S/N
|
Mwaka |
% ya Ufaulu |
1 |
2016 |
76.23 |
2 |
2015 |
71.07 |
3 |
2014 |
74.32 |
4 |
2013 |
53.76 |
Aidha mtihani wa kidato cha sita (ACSEE) asilimia ya ufaulu (Daraja la I, hadi IV) kwa mujibu wa tathmini ya matokeo ni kama ifuatavyo
Jedwali Na. 5: Ufaulu wa Kidato cha sita kuanzia mwaka 2014 hadi 2016
S/N |
Mwaka |
% ya Ufaulu |
1 |
2016 |
93.4 |
2 |
2015 |
99.6 |
3 |
2014 |
99.3 |
Katika mitihani ya kitaifa mwaka 2016 Halmashauri ya Meru imeshika nafasi mbalimbali kama inavyoonekana kwenye Jedwali lifuatalo.
Jedwali Na. 6: Nafasi za Kimkoa na Kitaifa
Kidato
|
Nafasi Kimkoa
|
Nafasi Kitaifa
|
Kidato cha II
|
01 |
06 |
Kidato cha IV
|
01 |
19 |
Kidato cha VI
|
Shule ya Kisimiri ilikuwa ya Kwanza Kitaifa
|
Katika kuhakikisha ufaulu unafikia asilimia 80 kwa kidato cha nne kama ilivyoainishwa kwenye Mpango wa Matokeo Makubwa sasa - BRN, Halmashauri inafanya jitihada mbalilmbali. Miongoni mwa jitihada zinazochukuliwa ni kurekebisha ikama kwa walimu wa masomo ya sayansi na hisabati, kutoa motisha kwa walimu kwa shule zitakazofanya vizuri kitaifa, kukamilisha ujenzi wa maabara za sayansi pamoja na kusimamia na kufuatilia kwa karibu ufundishaji shuleni.
1.7 Mpango wa Chakula
Shule zote 29 zimekuwa zikiendesha mpango wa chakula ambapo wazazi/walezi wanachangia huduma hiyo. Tangu utaratibu wa elimu bure kuanza huduma hii imekuwa haitolewi kwa ufanisi kwa kuwa baadhi ya wazazi wanaamini kuwa huduma hiyo inapaswa kutolewa bure. Shule zimehimizwa kupitia vikao vya bodi na wazazi kuhamasisha wazazi na kutoa elimu toshelevu kuhusu waraka wa elimu bure ili kukubaliana kwa kupitia mijadala ya wazi namna ya kuchangia huduma ya chakula kwa kuomba vibali Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pale ambapo huduma hiyo inahitaji mchango wa fedha.
1.8 CHANGAMOTO.
Zifuatazo ni baadhi ya changamoto zinazoikabili elimu ya sekondari katika Halmashauri ya Meru:-
S/N
|
CHANGAMOTO
|
MKAKATI WA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO.
|
1
|
Upungufu wa walimu Sayansi/Hisabati hivyo masomo hayo kutofundishwa ipasavyo.
|
Halmashauri imewasilisha mahitaji ya walimu hao wa sayansi TAMISEMI, kwa mwaka 2016/17 walimu 10 wameajiriwa.Shule zinahimizwa kushirikiana na wazazi kuchangia kuwalipa walimu wa sayansi na Hisabati wanaoajiliwa kwa muda ili kukabili uhaba.
|
2
|
Upungufu wa nyumba za walimu hasa kwa shule zilizoko pembezoni mfano Maruvango,Miririny,Mbuguni Makiba.
|
Bodi za shule na jamii zinahimizwa kutafuta wahisani wa kuchangia ujenzi wa nyumba za walimu.
Aidha jamii inahimizwa kuwatafutia walimu nyumba za kupanga zilizo jirani na shule. |
3
|
Kusuasua kwa huduma ya chakula cha mchana kwa sababu ya uelewa usio sahihi kuhusu wajibu wa wazazi kuendelea kuchangia huduma ya chakula kwa shule za kutwa.
|
Kutoa elimu kwa wazazi kupitia vikao vyao na kuomba vibali vya kuchangia ofisi ya katibu tawala mkoa.
|
4
|
Upungufu wa majengo ya utawala (administration blocks) unaosababisha shule 21 kutumia vyumba vya madarasa kama majengo ya utawala.
Upungufu wa samani za ofisi unaosababisha walimu kutumia viti na meza wanafunzi. |
Vipaumbele vya ujenzi vielekezwe kwenye ujenzi wa ofisi za shule na shule zitenge fedha kidogo kidogo kwenye fedha za elimu bure kwa ajili ya kununua samani za ofisi.
|
5
|
Wanafunzi wa kidato cha kwanza kutoripoti kwa wakati na wengine kuhamia shule zenye hosteli/bweni za Halmashauri nyingine za mkoa huu na nje ya mkoa au kwenda shule binafsi hivyo lengo la uandikishaji kutofikiwa kwa 100%.
|
Watendaji wa kata,maafisa elimu kata kuendelea kufuatilia walipo na hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya wazazi wanaozembea kuwaleta watoto wao shule.
Ujenzi wa mabweni au hosteli upewe kipaumbele kwenye mipango ya ujenzi wa miundo mbinu ya shule. |
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa