Halmashauri ya Meru ina eneo lenye ukubwa wa ekari 42 pembeni ya barabara kuu ya Arusha-Moshi umbali wa kilomita 11 kutoka katikati ya Jiji la Arusha. Eneo hili linahusisha pia eneo la maegesho ya mabasi madogo ya mjini (Town Buses) na Taxi (cabs).
Lengo la mradi ni kujenga Kituo cha mabasi cha kisasa (Morden Bus Terminal). Eneo hili limezungukwa na ekari nyingine 67 zilizotengwa kwa ajili ya miundombinu mingine kama vile Hoteli, Nyumba za kulala wageni (Guest House), Banks, Car Wash, Garage, Vituo vya mafuta, Zahanati, na Maduka.
Mpango huu wa ujenzi wa kituo kipya cha mabasi unafuatia agizo la Uongozi wa Mkoa wa Arusha kuagiza Halmashauri zijenge Vituo vipya vya mabasi nje ya Jiji la Arusha ili kupunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji.
Miundombinu ya maji, umeme iko jirani lakini pia eneo hili liko pembeni ya barabara ya lami (Arusha-Moshi).
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa