Halmashauri ya Meru imetenga eneo la ekari 25 kwa ajili ya kujenga Kituo cha Michezo cha kisasa katika eneo la Valeska.
Kituo kitakuwa na viwanja vya michezo ya Mpira wa Miguu (Football), Mpira wa Pete (Netball), Mpira wa Kikapu (Basketball), Mpira wa Meza (Table Tennis), Mpira wa Wavu (Volleyball), Ngumi (Boxing), Riadha, Hockey, Squash, Badminton, Golf nk.
Kituo hicho pia kitakuwa na kumbi za kisasa kwa ajili ya mikutano, vyumba vya madarasa, vyumba vya kulala wachezaji. Kituo hiki kikikamilika kinaweza kutumia fursa za timu mbalimbali zinazotaka kuweka kambi mahali penye utulivu na hali ya hewa nzuri kama ya Arusha.
Kituo hiki pia kinaweza kutumika kukuza vipaji kwa michezo mbalimbali kama vile Mpira wa Miguu, Riadha, Ngumi nk.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa