Halmashauri ya Wilaya ya Meru ina eneo linalolimwa zao la nyanya lenye hekta 1,460 kutokana na hali ya hewa inayofaa kwa zao hilo na upatikanaji wa mvua na maji ya umwagiliaji ambavyo vinachangia kustawi kwa zao hili. Zao hili linastawi na kulimwa kikanda kulingana na baadhi ya vigezo tajwa hapo juu.
Hata hivyo wakulima wa zao hili wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingi zikiwemo kupata hasara wakati wa mavuno kwa kukosa soko na bei nzuri, na pia mazao mengi kuharibika kwa kuoza kutokana na kukosa vifaa bora vya kuhifadhia.
Kata inayolima zao hili kwa wingi ni Ngarenanyuki yenye wakazi 20,379 ambayo iko kwenye ukanda wa juu wenye hali hewa nzuri na uhakika wa mvua kwa mwaka mzima. Kwa sasa eneo la ekari 1,200 zinazotumika kwa kilimo cha nyanya ambapo mavuno ni wastani wa tani 120,000 kwa mwaka.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa